News
Loading...

Baada ya mgomo wa madaktari, posho za wabunge zimekaa vibaya!


Mh Shibuda: Yeye alitaka posho iwe laki tano.
Mara nyingi nimetokea kuandika humu na katika mtandao wa Facebook nikiikosoa serikali kwa kuwaongezea posho wabunge toka sh 70,000/= mpaka sh 300,000/= huku wakiwapuuza madakatari, wauguzi, walimu na askari polisi. Ni dhahiri mgomo wa madakatari umempa Rais Kikwete kigugumizi cha mkono katika kutia sahihi yake kubariki ulafi huo. Na namuombea kwa Mungu Rais wetu apate nguvu ya kuutupilia mbali mpango wa kuwaongeza posho wabunge na pesa hizo ziende katika sekta ya afya kwanza na zingine zifuatie. Mwisho napenda kutoa rai kwa serikali na wa Tanzania kwa ujumla wetu """"tuwaunge mkono madaktari wapewe maslahi mazuri wanayostahili na yawe katika uwiano mzuri ambao hautoyumbisha uchumi wa nchi vile vile tusichoke kuwapigania wauguzi, walimu na askari polisi nao waangaliwe katika upande wa mishahara stahiki na mazingira mazuri ya kazi na makazi bora"    Mungu ibariki Tanzania!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :