News
Loading...

Charles Boniface Mkwasa anastahili sifa za kipekee


Wachezaji wa Twiga Stars wakishangilia moja ya magoli jumapili 
Kocha mzalendo Charles Boniface Mkwasa (Master) anastahili pongezi za juu kabisa kwa kukiwezesha kikosi cha Twiga Stars kucheza kama timu iliyofundishwa tangu utotoni. Pamoja na ushujaa wao wote Twiga stars imekuwa kama mtoto yatima ambapo Mkwasa amakuwa akilalamika kila mara akitaka timu hiyo ya wanawake anayoifundisha kwa takriban miaka miwili sasa ipewe udhamini kama ilivyo Taifa Stars ambayo na dhamini hizo nono bado imekuwa ikisuasua licha ya kuwa na wachezaji wa kulipwa. Nafikiri umefika wakati serikali kupitia wizara husika waingilie kati suala la timu hiyo ya Twiga ipate udhamini ili iweze kushiriki mashindano bila matayarisho duni kama lilivyo sasa. Twiga Stars ambayo jumapili iliyopita iliichakaza vibaya timu ya taifa ya Namibia kwa kuibugiza magoli 5-2 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na matokeo hayo ni baada ya kuwafunga madada hao wa ki Namibia magoli 2-0 jijini Windhoek wiki tatu zilizopita. Na sasa itapambana na Ethiopia katika mchezo wa kugombea nafasi ya kushiriki kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake hapo mwakani. Twiga ilionesha dalili nzuri ilipokwenda South Africa na Msumbiji mapema mwaka jana na kupata matokeo mazuri huko. Mungu ibariki Twiga Stars Mungu ibariki Tanzania.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :