Kushoto ni daraja linalounganisha Tabata external na Kigogo |
Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam maeneo ya Ubungo maziwa amekuwa akiishi katika hali hatarishi mno kama picha hizo mbili zioneshavyo. Nyumba anayoishi yeye na familia yake ipo ukingoni mwa daraja la maeneo hayo ambapo inaelekea kingo zake zimeathiriwa na mvua kubwa zilizonyesha mapema mwaka huu ambazo pia zilileta maafa makubwa maeneo ya mabondeni ambapo nyumba zaidi ya elfu moja ziliharibiwa na mafuriko hayo. Nyumba hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na viloba vya mchanga ili isianguke kama picha chini ioneshavyo. Leo nilipita eneo hilo na kumshuhudia dada mmoja akifagia katika nyumba ambayo kwa sasa inaonekana kama balkoni katika jengo la ghorofa. Nashauri viongozi wa serikali ya mtaa huo wachukue hatua za haraka kuihamisha familia hiyo kabla ajali mbayaa haijatokea hapo na tukaanza kumtafuta mchawi ilihali ukweli unajionesha.
0 comments :
Post a Comment