News
Loading...

TFF iondoe adha ya upatikanaji wa tiketi uwanja wa Taifa


Askari wa farsi akijaribu kutuliza ghasia katika gari la kuuzia tiketi
Pichani juu ndivyo ilivyokuwa katika uwanja wa taifa siku ya jumamosi siku Yanga ilipocheza na Azam Fc. Nashindwa kuelewa kwa nini TFF inaachia hali hii ngumu ya upatikanaji wa tiketi uwanjani, kwa mfano siku ya jumamosi palikuwa na gari moja tu kuuzia tiketi na kutokana na watu wanaotaka tiketi  kuwa wengi zinatokea fujo ambazo si za lazima. Na kwa jinsi wa Tanzania tulivyo si wastaarabu kila mmoja anataka apate yeye kwanza. Wengine hufanya fujo ili waweze kuwaibia wenzao basi alimuradi tabu tupu.
Labda mimi ningeshauri kama mtaalamu TFF wahakikishe wanaweka magari mengi ya kuuzia tiketi ili kuondoa adha hii ya upatikanaji wa tiketi kwa kuwa inaonekana hawana utaalam wa kutambua nini wafanye kuondoa usumbufu hapo.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :