News
Loading...

Mashahidi waanza kutoa ushaidi kesi ya Swetu Fundikira


Hayati Swetu Fundikira enzi za uhai wake.

Aliyevaa shati la bluu ni mtoto wa marehemu Misuka Swetu
 Jana jumatatu mashahidi watatu walianza kutoa ushahidi katika kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira, shahidi wa kwanza alikuwa Sostenes Mbuya ambaye ndiye aliyekuwa na marehemu katika gari lake siku ya tukio.Sosthenes alionesha umakini mkubwa katika utoaji wake wa ushaidi pamoja na hila nyingi za mawakili wa utetezi Bw Mruge na Mzee Mkongo. Hata hivyo mawakili walifanikiwa kumchokoza shahidi wa pili Ben Kinyaiya na hatimae Ben kujibu maswali kwa hasira mpaka Jaji Zainabu Mruke alipomkumbusha Ben kuwa hao ni mwakili na watajaribu kumchokoza shahidi ili apoteze mwelekeo, baada ya hapo Ben alirudi sawa na kujibu maswali kwa uthabiti. Shahidi wa tatu Ali Othman naye alipata kash kash za mawakili hao wa utetezi lakini aliendelea kujibu maswali kwa umakini mkubwa. Kesi itaendelea kusikilizwa leo kwa mashahidi wawili kutoa ushahidi. Kesi hiyo inasimamiwa ki ustadi mkubwa na Jaji Zainabu Mruke wa mahakama kuu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :