News
Loading...

Tuliponusurika kutegewa magogo barabarani!


Mmoja wa wahanga wa tukio la kusitisha safari baada ya kuwekwa magogo barabarani akisubiri pawe shwari kabla ya kuendelea na safari yake.
Alfajiri ya juzi kuamkia jana nikiwa na ndugu zangu tunatokea Tabora kuelekea Dar kwa gari dogo aina Toyota Mark X ghafla tukiingia kijiji cha Bwawani tukakuta msururu wa magari mengi (malori) yakiwa yameegeshwa pembeni mwa barabara baadhi ya watu waliokuwa nje ya malori hayo wakatusimamisha, tulipotaka kujua kulikoni ndipo tukaambiwa kuwa nje kidogo ya kijiji hicho cha Bwawani kuna watu wanaosadikiwa majambazi wametega magogo kwa dhamira ya kuteka magari na kufanya unyanganyi na kuwa tayari walishafanya mawasiliano na Polisi Chalinze kuwapa taarifa hiyo hivyo nasi tukaegesha pembeni na kuanza kusubiri. Baada ya kama nusu saa hivi ya kutoona gari la aina yeyote kupita tokea Chalinze tukathibitisha ni kweli paliwekwa magogo.

Baada ya dakika 40 hivi baadhi ya malori yakaanza kuondoka kuelekea Chalinze huku wakituambia majambazi hao wameshaondoka, lakini hata hivyo tukasita kuyafuata yale malori mpaka ikatokea Toyota Noah toka Chalinze ndipo sisi na wenye magari mengine tukaanza tena safari ya kuelekea Dar. 

Kilichoshangaza ni kutokuwa na kauli rasmi toka Polisi Chalinze kuthibitisha ni kweli majambazi wale walishaondoka eneo walilotega magogo. Zaidi ni matumaini yangu na wadau wengine kuwa serikali itaimarisha doria eneo hilo ambalo limetajwa kutumika mara kwa mara na majambazi hao.
Subira yavuta kheri
Gari nililokua nikiendesha toka Tabora
Malori yakiwa yameegeshwa pembeni

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :