News
Loading...

IMETOSHA! Henry Mdimu aanzisha harakati dhidi ya ukatili na mauaji kwa albino!


Balozi wa kujiteua Bw Henry Mdimu akisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo idara ya maelezo.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Bw Henry Mdimu leo hii mchana amezungumza na vyombo vya habari kuvieleza azma yake ya kuendesha harakati mpya iitwayo IMETOSHA kupinga ukatili na mauaji dhidi ya albino. Mdimu alisema kuwa harakati yake italenga zaidi katika kuelimisha jamii kuwa albino ni binadamu kama wengine na ana haki ya kutonyanyapaliwa ,kusemwa vibaya, kutemwa mate, kukatwa viungo na kuuawa. Vile Balozi Mdimu alieleza azma ya kamati yake ya kuandaa matembezi ya hiari siku ya jumamosi ya tarehe 21/3/2015 yatakayoanzia Leaders Club kuelekea Morocco, Manyanya, Kinondoni Road, Ali Hassan Mwinyi na hatimae kuishia Leaders club ambapo patafanyika mnada wa picha iliyochorwa na Ndunguru pia fulana zeneye neno IMETOSHA zitauzwa pale ili kupatikane pesa ambazo Balozi Mdimu na kamati yake watazitumia kwenda Kanda ya ziwa kufanya kampeni mijini na vijijini juu ya mauaji na manyanyaso dhidi ya ndugu zetu albino. Pia Henry Mdimu aliwapongeza rafiki zake ambao amekuwa nao bega kwa bega mpaka leo kwa kujitoa kufanikisha harakati yake mpaka sasa. Aidha aliongeza kuwa baadhi ya wasani wakiwemo Jhikoman, Profesa Jay, Mwana FA, Cassim Mganga, Fid Q, Ray C na Roma wamejitolea kurekodi wimbo mmoja kila msanii ambapo album itauzwa kutunisha mfuko utakasaidia harakati ya IMETOSHA huko kanda ya ziwa. Pia Bw Mdimu alipongeza Tanzania Bloggers Network kwa kujitoa kubeba kampeni ya IMETOSHA na kusisitiza kuwa makampuni yajitokeze kuunga mkono harakati ya IMETOSHA ili kuiongezea nguvu kampeni hiyo endelevu.
Balozi Mdimu akisikiliza swali toka kwa mmoja wa waandishi wa habari, kushoto kwake ni msanii Masoud Kipanya.
Toka kushoto Joachim Mushi(Mwenyekiti wa TBN) Monica Joseph(mjumbe TBN) Mdimu na Masoud Kipanya
Salome Gregory (Katibu IMETOSHA COMMITTEE)

Neema(kushoto) na Faridah Wajumbe IMETOSHA COMMITEE
Joachim Mushi mwenyekiti wa mtandao wa bloga Tanzania akitoa wito kwa waandishi wa habari waiunge mkono kampeni ya IMETOSHA kwa kunua fulana za kampeni hiyo kama aliyovaa yeye.

Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo kwa umakini
Chukua namba yangu: Somoe Ng'iitu (kulia)
Masoud Kipanya(Mwenyekiti) kamati ya IMETOSHA
Msanii Jhikomana kushoto na Salome Gregory
Monica Joseph akifafanua jambo leo MAELEZO

Kelvina na Masoud Kipanya
Msanii Kassim Mganga akihijiwa redio ya Dutch welle
Abrah, Mdimu na Masoud
Wajumbe wa kamati ya IMETOSHA Mkala, Mdimu, Masoud na Kelvina kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari leo mchana idara ya MAELEZO.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :