News
Loading...

Kamati ya IMETOSHA yaalikwa lunch Samaki Samaki!Afisa mkuu wa idara ya masoko ya mgahawa wa Samaki Samaki Bw Edward Lusala (kushoto) na Balozi Henry Mdimu.
Kamati ya IMETOSHA ambayo ipo chini ya balozi wa kujiteua Henry Mdimu leo hii mchana ilialikwa chakula cha mchana na menejimenti ya mgahawa maarufu jijini wa Samaki Samaki ambapo baada ya chakula afisa masoko Bw Edward Lusala alifanya mazungumzo na kamati kujua jinsi gani mgahawa huo unaweza kusaidia harakati ya IMETOSHA. Hata hivyo mazungumzo hayo yalikuwa ni ya awali katika mengi yatakayofuatia, yatafanyika tena siku za usoni kupata ufumbuzi wa jinsi gani mgahawa huo utajihusisha kwa ukamilifu. Blog hii kupitia mmilikiwa wake Bw Mkala Fundikira ameupongeza uongozi wa mgahawa huo kwa kuguswa na adha waipatayo ndugu zetu albino, na kuongeza kuyataka makampuni mengine yanapaswa kuiga mfano walioonesha samaki samaki ili kusaidia mapambano dhidi ya ukatili, manyanyaso na mauaji dhidi ya albino.
Kushoto Masoud Kipanya(mwenyekiti (IMETOSHA) Faridah, Neema na Cassim Mganga (wajumbe IMETOSHA)

Kushoto Cuthbert Kajuna, Kelvina, msanii Jhikoman na Masoud Kipanya LUNCH!
Kushoto Monica Joseph, Salome Gregory(Katibu IMETOSHA) na mjumbe Abrah.

Mhm chakula kitamu sana mpaka nasinzia!
Mlo jamani!

Picha ya pamoja baada ya chakula cha mchana mgahawani samaki samaki jijini Dar es Salaam.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Salome Gregory said...

Safari imeanza.