News
Loading...

Serikali kujenga daraja la kisasa!


Muonekano wa daraja jipya litakalojengwa tokea Coco beach kwenda Agha Khan Hospital 
Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ina mpango wa kujenga daraja jipya la Salenda kwa ushirkiano na serikali ya Korea, litakalopita baharini kuanzia Coco Beachi (Oysterbay) kwenda Hospitali ya Aga Khan (Maeneo ya Ocean Road/ Baraka Obama Road). Daraja hilo pamoja na barabara zake, litakuwa na urefu wa kilomita 7.2 na uwezo wa kupitisha magari zaidi ya 61,000 kwa siku huku likiwa na njia nne za magari pamoja service road njia za waenda kwa miguu kila upande.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Chung Il wapili kushoto kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu sekta ya Ujenzi pamoja na mchakato wa Ujenzi wa Daraja jipya la Salenda litakalopita baharini. Wa kwanza kushoto ni mke wa Balozi huyo.

Picha na habari Mtaa kwa mtaa blog

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :