News
Loading...

New Dar City 2025 Inawezekana!




Jengo hili linapendeza hasa baada ya kufanyiwa marekebisho
Hili ni moja ya majengo yalioachwa na Wakoloni, majengo kama
haya yamepotea kabisa baada ya wamiliki wa majengo jijini Dar
Kuyavunja yale ya zamani na kujenga mapya na ya kisasa zaidi. 

  

  
Jengo kama hili likifanyiwa matengenezo
litapendeza kamahili jingine hapo juu
ambalo ni jego linalotumiwa na TRA.


Sidhani kama unahitaji digrii ya nyuklia kujua kwamba
serikali zetu hasa za awamu ya pili na kuendelea
hazikuupa utamaduni nafasi yake, kwani waliiona Dar 
ikibadilika lakini wakaiacha ibadilike huku ikikua na
kupoteza sura yake ya miaka 30 tu iliyopita.Dar ya Leo
si Dar ya mwaka 1980,imebadilika mno. Ninachiokiongela
hapa ni kuwa palipaswa pawe na mipango ya kujenga
New Dar es Salaam kama ingekuwa ni Bagamoyo
au Mkuranga tusingejali alimuradi bahari ipo kwa wapenda
upepo wa bahari katika miji yote miwili niliyoitaja.
Kwa mfano mipango hiyo ingeanza mwaka 1990 leo hii
tungekuwa wapi na hiyo New Dar city? Ambayo ingekuwa
na majengo kama hayo hapo chini Vile vile bado tungekuwa
na Dar yetu ya miaka ya 60 na 70 kama ilivyo London
ambayo bado inayo majengo yake ya zamani na ina yale 
mapya eneo jingine, ingekuwa na majengo kama yale pale juu.
Any way hiyo ni missed opportunity kwa waliopita, Dada yangu
Mh Anne Tibaijuka anayo nafasi ya kufanya hivyo na nafikiri
ana mtazamo chanya juu ya makazi bora na hii na inatokana
na kazi aliyokuwa akifanya huko UN habitat.Kazi kwako Mh Ane
Tibajuka.




 
New Dar city ingekuwa imepambwa na majengo kama haya na huu
ndio ungekuwa muonekano wake kwa juu, tungekuwa tumepiga
hatua kubwa mno hasa katika kupunguza msongamano wa magari
na ujenzi holela wa makazi hasa maeneo ya mabondeni.



  

 

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Anonymous said...

Haya ni mapungufu makubwa ya wasimamia mamlaka husika ktk hili ! mfano wa jengo uliloonyesha kwenye hiyo kona ya mtaa wa samora na huo unaokwenda shule ya forodhani ! hilo ni jengo zuri sana linaonyesha Architectural ya kale na likikarabatiwa linakuwa zuri sana na huo mtaa wa samora kuna majengo mengi sana ambayo ni ya kale lkn yanabomolewa kwa kasi bila kujali historia ya jiji letu ! Kama mtu kweli anataka wekeza akajenge kule bunju,kibada nk ambapo kuna nafasi ya kutosha na sio hapo tena ambapo mifumo ya huduma muhimu imeshazdiwa.
Kassembo