News
Loading...

Big Up Ilala


Vijana hwa wakiondosha vifusi vya mchanga katka barabara
ya Ally Hassan Mwinyi leo asubuhi
    

Hivi ni baadhi ya vifusi vya mchanga vilivyotapakaa Br
Ally Mwinyi leo asubuhi kabla havijaondolewa mchana huu.
  Leo hii asubuhi nilipita Br Ally Hassan Mwinyi kuelekea mjini nikiwa njiani maeneo ya jamatini nikaona vifusi vidogo vidogo vya michanga vikiwa pembezoni mwa barabara hiyo, nikavipipiga picha kwa madhumuni ya kuviandikia makala kwa kuwa ni kawaida vifusi kama hivi hutolewa katika mifereji ya maji kisha huachwa hapo hapo mpaka vifusi hivyo hutawanyika na kurudi tena miferejini. Kwa mshangao wangu na mwingine yeyote aliyeona vifusi hivyo asubuhi, nikitokea mjini kuelekea selander bridge nikakuta lori dogo aina ya Toyota Dyna imeegeshwa pembezoni mwa barabara huku kukiwa na vijana wapatao wanne hivi wakizoa vifusi vile kwa kutumia sepeto na kuvitupia garini, nikasema si HABA. Kama hawa walikuwa ni wahusika wakiondosha vifusi hivyo au ni mtu tu mwenye shida na mchanga ule, mimi na wewe hatujui ila kilichomuhimu kwetu sisi ni vifusi vile kuondoshwa katika pembe zile za barabara hiyo. Labda niseme hongera kwa kutimiza wajibu wenu wahusika katika wilaya ya Ilala pamoja na Voingozi wenu. Big Up Ilala!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :