News
Loading...

Traffic lights za nini hapa?
Taa nyekundu imeka kuashiria kuwa magari
yasimame kupisha mengine yapite, lakini picha
 ya chini inaonyesha magari yakiendelea kupita
kana kwamba hapana taa hizo pahala hapo.
Hapa ni makutano ya Br Kawawa na Br Kinondoni, pana taa za kuongozea magari lakini zimekuwa zkipuuzwa na madereva wapitao hapo na magri yao, ama wameambiana au wote wanapajua pahala hapa kuwa ni pa kupita tu. Na pamekuwa pakigongwa wenda kwa miguu mara nyingi tu, hasa nyakati za usiku. Nawaomba wahusika wapatupie macho mahala hapa kabla hapajageuka kuwa machinjioni. Ikiwezekana pawekwe askari wa usalama wa barabarani hapo hasa siku za wikiendi wapige mabao kwa siku nzima ili kuwakumbusha waendesha vyombo vya moto kuwa hapo ni Kinondoni na ni sehemu ya Tanzania ambako pana serikali na sheria zinafuatwa, na si Peshawar Kaskazini ya Pakistan ambako ni maarufu na panafahamika kuwa hakuna serikali wala sheria inayofuatwa huko. 


Gari kadhaa zikikatiza makutano ya Br za Kawawa na Kinondoni
huku taa nyekundu ikiwa imewaka kuashiria kuzisimamisha ili
kupisha nyingine zinazotoka Kinondoni Rd zipite.
FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :