Hii si ile barabara mbovu bingwa nchini ya kutoka Itigi kwenda Tabora, la hasha hii ni bara bara ya kutoka Mikocheni Chama kwenda Msasani Macho(Ccbrt) barabara hii imekua adha kwa wanaoitumia na kwa wakazi wa Bonde la Mpunga. Imekuwa katika hali hii na zaidi ya hii pengine kwa miaka mitano sasa. Jitihada kadhaa zimefanyika kuifanya ipitike kirahisi hasa vipindi vya Masika lakini wahusika wamekuwa aidha wakikwepa ukweli au kutojua ni nini kinahitajika kufanywa pale,lakini mimi kwa umbumbumbu wangu wote nilio nao lakini nafahamu pale panahitajika mfereji mkubwa upeleke maji baharini ambapo ni kama mita 500 toka ilipo barabara hii. Kazi kwenu wahusika na masika ndio hiyo yabisha hodi.
Sio Itigi hapa

1 comments :
Hi barabara ni kiungo kizuri sana kati ya barabara ya Msasani/Mikoroshoni kupitia Msasani Fish market na Old Bagamoyo ! na kama itatengenezwa vizuri husaidia sana kukwepa msongamano wa magari,kipindi kilichopita palitengenezwa kwa kuweka kifusi na open drainage channel lkn mvua zilizopita zilipaharibu kabisa na sasa naona kuna jitihada zingine lkn ni muhimu waweke lami kabisa na The contractor should be supervised intensively and consultants also have to design appropriate design.pasipotezwe pesa za serikali bure hii njia nzuri sana kwa kukwepa msongamano wa magari !.
Kassembo
Post a Comment