News
Loading...

Kilio changu hatimaye kimesikika!


Picha hii niliichukua tarehe12/10/2010.
Mpenzi mdau kama unakumbuka picha hii hapa kushoto niliiweka katika makala iliyokuwa na kichwa  "DAMPO KATI KATI YA MAKAZI" imewachukua watu wa Halmashauri takriban miezi miwli na wiki zipatzo mbili hivi kuja kuondosha taka taka zilizokuwapo hapo. Kuna msemo wa Kingereza usemao Justice delayed justice denied yaani Haki ikichelewa kutendwa basi ni sawa na kuwa haikutendwa. Nikisema hivi namaanisha kuwa wakazi wa eneo hili ni haki yao kuwa na eneo safi kama lionekanalo katika picha ya hapo chini kushoto wakati wote si kwa nyakati fulani fulani tu. Watu wa halmashauri ya wilaya ya Kinondoni wanapaswa wawe na utendaji endelevu wa kuisafisha halmashauri hii chafu, mfano mzuri ni hii picha hapo chini kabisa. Inaonesha tela lao limeandikwa pendezesha manispaa yako lakini tela hilo limezungukwa na taka za haja, lakini je huu ndio upendezeshaji wanaou himiza au kuna mwingine? Kama wahimizaji hawatimizi majukumu yao hali hiyo itaendela kujirudia mara kwa mara.
  Picha hii nimeichukua leo alhamisi 
tarehe 27/01/2011
PENDEZESHA MANISPAA YAKO 
 kauli mbiu hii inatekelezwa haswa!FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :