News
Loading...

Mfereji mkubwa ndio jibu!



Mpendwa mdau barabara hii hapo chini pichani ni ile itokayo Mikocheni Tanesco kwenda Msasani Macho(CCBRT) nilipata kuiandikia makala yenye kichwa SIO ITIGI HAPA! mnamo tarehe 14/12/2010 kuwa wahusika hawatambui umuhimu wake labda kwa kutoitumia au kutojua nini cha kufanya mahala hapo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza kwa watumiaji wa njia hiyo nyakati za masika, ambapo ikijaa maji watumiaji hasa wenye gari ndogo hulazimika kuzunguka Namanga ili waweze kufika upande ama wa Tanesco Mikocheni au CCBRT al maarufu Macho. Katika pita zangu nimekuta pamejazwa vifusi vya udongo na mawe, jitihada ambazo hazikufahamika mara moja ni za nani manispaa au wakazi wa Bonde ka mpunga. Lakini bado pahala hapo hapajapatiwa ufumbuzi wa kina, kwani masika ikianza itabeba tena kifusi hicho kama vingine vingi vilivyowahi kuwekwa hapo. Narudia tena, kwa elimu yangu ya Kuzaliwa Dar Chuo kikuu naona hapa panahitaji mfereji mkubwa wa kupeleka maji baharini sio vifusi au vimtaro Uchwara kama hicho hapo pichani chini kabisa.

Jinsi ilivyo sasa

 

Ilivyokuwa  tarehe 14/12/2010

 
Huu ni mfereji mdogo ambao hautokidhi
mahitaji ya maji ya mvua za masika
kwenda baharini.

 

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :