News
Loading...

Msanii wa wiki!
AY kazini.
 
AY akionyesha moja ya mavazi
yenye nembo yake yeye mwenyewe.


Kofia na fulana ni mazao
mengine ya AY katika
 ubunifu wake.
Unapozungumzia Muziki wa Bongo Flava huwezi kuacha kumtaja Ambwene Yesaya AY ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika kuuweka muziki huo hapa ulipo sasa ambapo unakubalika na watu wa rika zote ndani na nje ya Afrika Mashariki na kati. AY ambaye alikuwa mmoja wa wasanii kadhaa waliounda kundi la East Coast kwenye miaka ya mwanzoni ya 2000 alijiengua toka kundi hilo kwa sababu kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kutaka kufanya kazi kama yeye na tumeyaona mafanikio yake mpaka sasa nayo ni pamoja kumiliki nembo yake ya mavazi na kuwa ni msanii anayejipanga mno pengine kuliko yeyote hapa Tanzania kabla ya kufanya kazi yeyote ile, iwe audio, video na hata ile ya ubunifu wa mavazi. Kwa kifupi yupo kikazi zaidi. Pia ni msanii mwenye connections nyingi ndani na nje ya nchi jambo ambalo limemsaidia mno katika kufikia mafanikio anayoyapata kama kupata shows duniani kote na kupata matangazo ya kila aina. Kwa kifupi mahali ambapo nina hakika AY hajawahi kufanya show ni mwezini tu! Na yafuatayo ni mahojiano mafupi kati yangu na AY aka Mzee wa Commercial:


Mambo AY?
Poa za mwaka mpya kaka?
Si mbaya ndugu yangu, namshukuru Mungu. Sasa nina maswali machache nahitaji kukuuliza na majibu yako yatawafaidisha wadau wa blogu hili na wale ambao ni washabiki wako waliopo pande zote hapa ulimwenguni. Na naanza hivi:

1.Ni uhusiano wa auna gani umewahi kuwa nao na Amani? (msanii m Kenya)
Tuliwahi kuwa wapenzi hapo nyuma lakini kwa sasa tumebaki kuwa marafiki wa kawaida.
2.Huu ni mwaka mpya wa 2011 washabiki wako wategemee nini?
Kama kawaida sipendi kuongea sana, ila natarajia kufanya kazi zenye kiwango cha juu sana kuliko ambazo nimeshafanya, i  will shortly shift gears to the higher levels!
3. Una single yoyote mpya na tuitegemee lini kama ipo?
Bila shaka ipo na nitatoa video wiki hii, wimbo unaitwa Good Look, nimemshirikishaMiss Trinity toka California, US of America. N video hiyo 
4.Audio ya wimbo huu imetengenezwa na kampuni gani?
Imetengenezwa na B Hits chini ya producer Hermy B.
Basi nashukuru sana kaka tutajiona next time all the best!
Nashukuru sana kaka, pamoja sana!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :