News
Loading...

Tanzania bado ni kisiwa cha amani?


Mh Rais Jakaya Kikwete
awajibishe watendaji wake.
Baada ya machafuko ya Arusha siku ya jumatano iliyopita, ambayo yalipelekea askari polisi kuua raia wanne wasio na silaha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya kwa risasi za moto. Mambo haya yametokea hapa Tanzania panapoitwa kisiwa cha amani na nchi inayoheshimika duniani eti kwa haki za binadam. Ina maana askari hao walikosa mbinu zote za kutumia hadi wakaona watumie risasi za moto dhidi ya watu wasio na silaha?

Haipingiki kuwa kukaidi amri ya chombo cha dola tena hasa cha nchi kama Tanzania inayovaa ngozi ya kondoo mbele ya jumuiya ya kimataifa na ya chui hapa nchini pale hata wanafunzi wakiandamana, ni hatari sana. Inavyofahamika CHADEMA walikuwa wanafanya maandamano ya amani huku wakiwa na vitambaa vyeupe kusisitizia hilo la amani. Bado nawapata CHADEMA na kosa la kukaidi amri ya polisi waliotaka maandamano hayo yasitishwe mara moja. Kwa upande mwingine upande unajiuliza viongozi wa askari wale hawakuwa na busara hata chembe? Tukio hili nalifananisha na lile lililotokea ijumaa ya januari 22/2010 ambapo askari jeshi (JKT) watatu, wa kiume wawili na wa kike mmoja walimpiga kijana mmoja maeneo ya Kinondoni studio mpaka akapoteza fahamu na hatimaye akapoteza maisha yake katika hospital ya Muhimbili saa zipatazo 30 baadae kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kichwani. Inaonyesha tu jinsi askari wetu walivyokosa busara, badala ya kutulinda pamoja na mali zetu wamekuwa ndio wauaji wetu. Halafu bado Mh Rais analiita tukio lile kuwa ni la bahati mbaya? Angeuawa mwanae angediriki kutamka hayo? Unapotumia chombo cha moto kama bunduki kuua na kujeruhi watu watu wapatao 17 kuna bahati mbaya hapo? Hii yote inatokana na ushabiki wa kisiasa ambao vyombo vya dola vimeendelea kuwa nao na kuukumbatia.
Natumai wale wote waliohusika na mauaji na udhalilishaji uliotokea Arusha jumatano watafikishwa mahakamani. Pia nataraji wahisani waibane serikali ili RPC wa mkoa huo awajibishwe na pia asubiri kupelekwa mahakamni kwa kutumia madaraka yake vibaya na kupelkea machafuko hayo.

Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mh waziri wa mambo ya ndani Shamsi Vuai Nahodha wakae wajiulize tukio kama hili kwa nini halitowahi kutokea katika nchi kama Uingereza? Najua wanafahamu jibu lake basi na hapa tufikie huko.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :