News
Loading...

Tunapangisha karibuni nyote!Mtazamo wa SSTL house kwa mbele
Hili ni jengo jipya na la kisasa linalomilikiwa na SSTL GROUP ambalo lipo Kinondoni "B" mtaa wa Dunga. Kama lionekanavyo na tangazo hapo mbele lina ghorofa tatu na sehemu ya chini (ground floor) zote zinapangishwa kwa bei nzuri (affordable prices), na zitawafaa wenye kutaka kufungua matawi ya benki, mashirika yasiyo ya kiserikali na ofisi zinginezo kama mashirika ya simu za mkononi nk. Jengo lipo sehemu nzuri inayofikika kirahisi kwa barabara iliyo katika kiwango cha lami. Kwa ndani ya kila floor kuna ofisi mbili hadi tatu, ambazo zinaweza kutumika kama ofisi za mkurugenzi, meneja, mhasibu nk. Kuna vyoo na jiko katika kila floor Chini pana maegesho ya gari zisizopungua kumi na tano hivi. Pia mmiliki wa jengo hili la kisasa kwa kutambua matatizo tunayoyapitia sasa nchini ya ukosefu wa nishati nyeti ya umeme ameweka jengoni hapo kifua umeme (generator) kikubwa na chenye ubora wa hali ya juu kabisa lakini chenye mlio wa chini mno ambacho kina uwezo wa kukidhi mahitaji ya jengo hilo lote kwa wakati mmoja. Vile vile kifua umeme hicho chenye kujiunganisha chenyewe mara umeme wa Tanesco unapokatika ni kipya kama lilivyo jengo lenyewe. Wahi sasa floor zenyewe zipo nne tu! Kwa mawasiliano zaidi piga simu no: 

Tel +255 222760037-8
Tel +255 222762429
Fax+255 222760293 
email-sstl@sstl.co.tz

Huu ni mlango wa mbele wa kuingilia jengoni.

Hii ni moja ya floor zinazopangishwa kwa ndani.Kiboko ya Tanesco na mgawo wao!

Hii pia ni floor nyingine kati ya nne zinzopangishwa.


Jiko halikuachwa nyuma.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :