News
Loading...

Vitanda 705 vya hospitali!


Naibu waziri wa Fedha na Uchumi

Top man Mh Mustafa Mkulo MB.
Tarehe 16/december/2010 niliandika makala juu ya wajawazito katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete kulazwa wawili hadi watatu katika kitanda kimoja siku hiyo ambapo wodi ya wazazi katika hospitali hiyo ina uwezo wa kulaza wajawazito kumi tu kwa wakati mmoja na pana idadi hiyo hiyo ya vitanda wodini humo. Kwa kweli hilo ni jambo la kusikitisha mno hasa ukizingatia kuwa wajawazito wanakosa vitanda kwa kuwa eti serikali haina pesa za kununua vitanda vya kutosha katika wodi hiyo wazazi lakini serikali hiyo hiyo ina pesa za kunulia magari ya mawaziri wake kama nilivyolishuhudia gari la waziri mdogo wa Fedha katikati ya jiji la Dar siku kadhaa zilizopita ndipo nikaamua kufanya utafiti mdogo tu ili nijue kitanda kimoja cha hospitali ni pesa ngapi halali za nchi hii na gari hilo lina gharama gani. Ndipo nilipofahamishwa kuwa sh laki mbili na nusu (250,000) ni gharama za kitanda kimoja. Full kipupwe Land cruiser Vx, 2010 Model, liliigharimu serikali yetu lofa kiasi cha takriban milioni mia moja na themanini hivi (180,000,000). Na hapo halijapelekwa service kila mwezi. Nikamtuma kijana  wangu anifanyie hesabu chap chap akanambia kwa pesa hiyo kama serikali ingeamua isimnunulie waziri mdogo wa fedha Bw Gregory Teu Land Cruiser ile, pesa hiyo ingeweza kununua vitanda visivyopungua 705 kwa bei ya sh laki mbili na hamsini (250,0000) kwa kila kitanda. Labda na tatizo la vitanda lingeondoka kabisa katika mahospitali yetu hapa nchini, kwa kuwa Kitete Tabora vilihitajika vitanda 20 tu hivyo basi vingebaki vitanda 685 ambavyo vingesambazwa nchi nzima. Je baada ya takwimu hizi unajisikiaje juu ya serikali yako pendwa?  Inawajali wananchi wake eh?

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :