Hii ni barabara ya Lumumba mjini Tabora, ambayo inafanyiwa matengenezo lakini cha ajabu magari yameendelea kupita hapo kiasi cha kutawanya changarawe zilizomwagwa hapo barabarani pamoja na kuwa pana tangazo kuwa njia hiyo imefungwa kwa matengenezo. Sijui wahusika wako wapi kuhakikisha kuwa barabara hiyo haitumiwi mpaka matengenezo yatakapokamilika vinginevyo itakuwa ni ufujaji wa pesa za Manispaa ambayo italazimika kulipa watu ili kurekebisha tena hizo changarawe.
Gari mojawapo inaonekana ikipita katika barabara ya Lumumba
0 comments :
Post a Comment