News
Loading...

Kumtaja mtu kwa rangi yake ni makosa kisheria!


Hii makala ndiyo ninayizungumzia.
Gazeti moja la kila siku leo hii limetoa makala yenye kichwa "Mzungu aisaidia jezi,mipira Twiga Stars" Kitu hiki ni makosa makubwa na kwa baadhi ya nchi zilizoendelea kosa hili linaweza likakufanya ukanyee debe japo kwa miezi sita au ukalipa faini kwa mahakama na fidia kwa mlalamikaji.Hebu fikiria wewe Mwafrika mweusi ukiwa katika nchi ya watu weupe halafu mtu akakuuliza kwa nia nzuri tu labda aseme " We mtu mweusi umetoka nchi gani Africa? utajisikiaje? Hapa nchini kwetu vitu kama hivi hudharauliwa lakini kwa wenzetu unaweza ukakuta unamtajirisha mtu hivi hivi.Tena basi baadhi ya watu katika kuonesha mapungufu katika peo zao wamediriki mpaka kuchapisha fulana zenye maandishi "MZUNGU" ili ujue machungu ya chchote ni mpaka kikutokee wewe. Tuseme unaingia super market ya Sainsbury's pale London, England unakuta fulana zinauzwa mle ndani zimeandikwa "Black Man au Negro" Utajisikiaje? Hata hivyo sidhani kuwa mwandishi wa habari husika na mhariri wake walifanya kosa hilo kwa makusudi bali hawakujua ni jinsi gani wangeumiza hisia za mtu mweupe atakayesoma makala ile.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

Anonymous said...

Duh jamaa angeona hiyo makala angewza hata kuahirisha kutoa msaada huo kwa timu yetu ya taifa ya wanawake!

Anonymous said...

Yes wamekosea, lakini ni Honest mistake tu!

Anonymous said...

Siyo "Black Man", bali ni "Negro" au kwa nchi za Scandinavia, Watu Weusi huwa wanajulikana kam "Neger".