News
Loading...

Wanawake tahadharini vyama vya siasa!


Spika wa Bunge
Kwa mtazamo wangu wa kibwege naona kama wanawake wasipokuwa waangalifu watatumika na vyama vya siasa ili vionekana kuweka uwiano kati ya wanaume na wanawake katika nafasi zakutoa maamuzi lakini labda si hasa dhamira yao, kwa mfano mimi siafiki utaratibu uliotumika kumpata mgombea wa kiti cha spika wa ndani ya CCM ambao uliekea zaidi katika kumbana Samuel Sitta asirudi bungeni kama spika.Sasa huko ni kuwapa nafasi wanawake wagombee nafasi za kutoa maamuzi? Au ni kuwawezesha washike nafasi hizo?  shaka ipo pale kamati kuu ilipotangaza kuwaengua wagombea wanaume na kuwaacha wale wa kike ambao walikuwa ni Anne Makinda ambaye alishinda,Anna Abdalla na Kate Kamba. Kama hilo halikuwa zengwe kwa nini uamuzi huo usingetangazwa kabla ili wagombea wanaume wasingefikia hata kuingiza majina yao katika kinyang'anyiro hicho. Halafu wanakaa na kulaumiana mambo yanapokwenda mrama lakini ukweli kwetu sisi wananchi ni kuwa CCM imekuwa haiishi kujipiga risasi miguuni kila linapotokea kubwa nchini. Kupotea kwa imani ya Wananchi kwa serikali ya CCM kunatokana na wao wenyewe kutuchukulia POA sisi ambao ndio mabosi zao na tumewatuma tu watufanyie kazi zetu, lakini wao sasa ndio wamekuwa ma boss. Kumbania Mh Samuel Sitta asirudi bungeni kama spika ni risasi moja wapo waliyojipiga. Sasa watu hawa walifikiri Wanachi hawakuona alichokuwa anafanya Sitta Bungeni? Yanashangaza kweli baadhi ya maamuzi yao! Lakini kikubwa je yanatoa picha gani kwa Wapiga kura?  
Hivi CCM hukaa wakajiuliza? Sidhani!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :