Hili ni jengo la makazi ya askari Polisi Msimbazi.
Hali hii ya ya makazi ya askari mahala hapa si nzuri kabisa sijui wizara ya mambo ya ndani inasemaje kuhusu uchakavu wa jengo hili lililo katikati ya jiji maeneo ya Kariakoo city. Au ndio wimbo ule ule serikali haina pesa? Kwa kuangalia tu mtazamo wa jengo hili je unaweza pata huduma safi yenye kiwango kutoka kwa askari anayeishi humu ambaye amesahauliwa na mwajiri wake? Kutopata maslahi bora toka kwa mwajiri wao hapatosaidia udhibiti utovu wa nidhamu katika jeshi hilo lenye dhamana ya kulinda raia na mali zao.
1 comments :
Hayo majumba yakifanyiwa ukarabati tu yatarudi kama mapya na kupendezesha mji.
Post a Comment