News
Loading...

Udugu wa Yanga na Toto una nafasi ya kutoa bingwa?


Kikosi cha timu ya Yanga
Jana nilibahatika kusikiliza kipindi cha michezo kupitia redio ya Tbc taifa nafikiri, akahojiwa kiongozi mmoja wa timu ya Toto Afrika na kuulizwa " Timu yako na Yanga ni ndugu, mkiwa tayari  mmejihakikishia kubaki katika Vodacom Premiership ya msimu ujao mtakuwa na haja ya kucheza kwa nguvu katika mchezo dhidi yao? ukizingatia wao watakuwa wanazihitaji pointi tatu ili wajiweke vema katika msimamo wa ligi na pengine kutwaa ubingwa. Akajibu kuwa kweli timu hizi mbili ni ndugu lakini tutacheza mechi hiyo ili kujiwekea heshima. Kwa mtazamo wangu hili suala la undugu katika mashindano TFF wanapaswa waliangalie vema. Kwanza maana yake ni nini? Nafikiri ni mwanya wa rushwa katika soka, na soka letu linanuka rushwa kila mtu anajua hilo. Msimu huu Yanga na Simba wanagombea kutwaa ubingwa wa Vodacom Premier League timu zote mbili zimefungana kwa pointi na kutofautiana kwa goli 1 ambapo Yanga ndio inaongoza ligi hiyo. Ndio maana natabiri mchezo mchafu utatembea na kutupatia bingwa msimu huu. Tusubiri tuone!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :