News
Loading...

Ajeruhiwa vibaya baada ya kutegewa kamba Isevya Makaburini!


Alex Ntonge akiwa wodini Kitete.
Kijana Alex Ntonge ambaye ni mwanachama wa Ukurasa wa Tabora ndio kwetu katika mtandao maarufu wa Facebook akiwa katika pikipiki yake akitokea katika starehe zake majira ya saa 8 za usiku alitegewa kamba na majambazi maeneo ya Isevya makaburini na  hivyo kupelekea kupata ajali mbaya iliyomsababishia majeraha kadhaa ya usoni kama ionekanavyo pichani kulia pamoja na baya zaidi la kuvunjika taya. Alex alitarajiwa kutoka hospitali ya Kitete leo hii ambapo anatarajia kwenda Nkinga Hospital kwa uchunguzi zaidi wa majeraha yake. Alex ambaye kwa sasa hawezi kuongea baada ya kufungwa nyaya katika meno yake ameweza kuwasiliana kupitia mtandao na kusema kuwa tiba hiyo ya nyaya itamfanya kutoweza kuongea kwa muda wa wiki sita atakapoondolewa nyaya hizo. Tukio hili lililomtokea Alex si la kwanza mahala hapo, pameripotiwa matukio mengi ya aina hiyo inashangaza tu pale Jeshi la polisi linavyolichukulia swala hilo. Labda watalipa kipaumbele mpaka watakaposikia kafa mtu kwa kutegewa kamba Isevya makaburini. Na pia inashangaza tupo katika miaka 50 baada ya Uhuru bado mkoa huu unategemea hospitali ya Taasisi isiyo ya kiserikali kwa tiba mbadala. Kazi kweli kweli!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :