News
Loading...

Guest House ya ajabu Urambo!


Msukosuko wa pasi wawashangaza wasanii
Siku ya jumapili nilikuwa Urambo na wadogo zangu Amini, Hmbizo, Nash D na Bekah ambao baada ya kukonga nyoyo za wakazi wa Tabora katika Miss Tabora walipata mualiko mjini humo kwa ajili ya kufanya show. Wenyeji wetu wakatufikishia katika nyumba moja ya wageni iitwayo Felan Guest House. Ulipowadia muda wa kwenda ukumbini vijana wakaanza kujiandaa kwa kunyoosha nguo zao , hivyo wakaomba pasi wakajibiwa na mhudumu wa kike kuwa hawana pasi hapo la wangeweza azima mahali ingekuwa vema. Kwa bahati mwenyeji mmoja anaishi karibu na Felan guest house akwaletea vijana pasi, na mimi ndiye niliyeenda nje kuifuata,. Nikiingia nayo ndani mhudumu wa kiume akanisimamisha na kuniuliza pasi ya nini? Nikamwambia akasema hapa hakuna ruhusa ya kutumia pasi! sikuamini nilichokisikia, nikamuuliza unasema? akarudia pasi haziruhusiwi humu ndani. Basi tukabishana pale nikaona hatungefikia mwafaka. Nikaona ni bora tuhame pale twende ambapo tutapata huduma ya pasi, lakini pia tulikuwa hatujalipia vyumba hivyo, nikaona nivema nikaitaaarfu polisi kwanza kabla ya kuhama ili tuwe salama kisheria. Nikafanya hivyo na nikapewa askari watatu kwenda tuhamisha. Tulipofika pale askari wakamhoji akakiri kutunyima huduma hiyo na akawa radhi tuhame bila kulipa chochote lakini akatakiwa akubali kimaandishi kuwa ameridhia. Hayo ndiyo ya Urambo kaeni chonjo na gesti husi hiyo. Pia nashauri wenye magesti wataje masharti yao kwa wateja wao kabla hawajaingia kupanga chumba ili hili lisijirudi

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Subi said...

Ajabu na kweli.
Vijimambo vya Tabora!