News
Loading...

Kwa jinsi tunavyoijua mentality ya wenyeji wa mashariki ya kati!


Osama Bin Laden.
Mpendwa mdau mimi wewe na yule sisi sote tunaijua mentality ya Warabu, awe Mpalestina awe Msaudia, alimradi akishajitolea kuwa yeye anaamini hivi au vile kujitoa uhai ni kitu kidogo sana. Tumeyashuhudia septemba 11 tumeayaona England julai 7 na kwingineko kwingi. Watu hawa wapo radhi kujitoa uhai kwa wanachokiamini iwe sisi wengine tunakiona sicho ndicho au la. Swali langu ni hili: Osama Bin Laden kwa kujiamini kiasi gani hata hakuwa hata na wembe wa kujikatia mishipa ya damu mara aliposikia ngurumo za helikopta wachilia mbali kuwa na Ak 47 au Bareta? Hivi inaingia akilini kweli kuwa alikuwa ameng'anganiana na mkewe ndipo akapigwa risasi ambazo zikamjeruhi na mkewe? Kwa jinsi niijuavyo akili ya watu wa aina yake asingetoa mwanya kwa Wamarekani wamuweke chini ya ulinzi akiwa hai, asingesubiri waje wavunje mlango wa chumba chake wamdhalilishe mbele ya mkewe. Tunayaona hayo mpaka katika filamu zinazotengenezwa Hollywood, labda White house ieleze vizuri tu, ni jinsi gani Osama alikufa.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Anonymous said...

Kaka huo ushabiki tu, Osamba is dead, walishamua sasa wewe unataka kubishana na mtoto wake au mkewe? au unataka kubishana na kundi lake lenyewe walio confirmed kuwa Osama amekufa....huo ni ushabiki wako wa udini tu. Acheni hayo.

Mkala26 said...

Mdau wangu labda hukusoma na kuelewa nilichokuwa nakitilia shaka mimi, ambacho ni je Osama aliuawa na Wamarekani au alijiu? Hakuna hata neno moja linalokataa kuwa amekufa katika makala yangu na mwisho nimesema "labda white house waeleze ni jinsi gani Osama alikufa. Maoni yako yamenisikitisha kidogo ku suggest udini wangu ndio unanifanya nishabikie suala hilo. Labda kama wewe ni mgeni na blog hii, mimi sijali wewe ni dini gani au kabila gani nitaandika chochote kinachonitatiza, na suala la jinsi alivyokufa Osama bado lina utata. Kuhusu udini, mimi sitoingia katika mjadala huo. Naomba soma vizuri article yangu na ukiielewa nitake radhi kama ishara ya ukomavu wako kidemokrasia.