News
Loading...

Chuki na dharau sasa ni dhahiri bungeni!


Mh Tundu Lissu Mb

Mh Frederick Werema
Mijadala mikali inayoendelea bungeni katika kipindi hiki cha bunge la bajeti inaelekea kuibua chuki na dharau miongoni mwa wabunge hasa wa CHADEMA na mwanasheria mkuu Bw Frederick Werema, Kwa mfano Bw Werema alithubutu kusema baadhi ya wabunge wanaongea tu ili waonekane katika runinga lakini wanachokiongea hakina mantiki, alisema hayo baada ya Mh Tundu Lissu kutaka kamishna na watendaji wa serikali kuondolewa madaraka ya kusamehe kodi, Lissu alilieleza bunge kuwa baadhi ya watendaji hao wanatum,ia vibaya madaraka hayo kiasi cha kusababisha rushwa na ufisadi. Baada ya mapendekezo hayo ya Mh Lissu ndipo mwenyekiti wa Mh Anne Makinda kumtaka  alipomtaka mwanasheria mkuu wa serikali kutolea ufafanuzi suala hilo ndipo Jaji Werema akasimama na kusema " Sina nia ya kumtukana mtu, lakini niseme tu hilo lipo wazi, kwamba mtu anaweza kuchelewa kulipa kodi, lakini ana sababu, sasa tunasema ikitokea ana sababu za maana, asamehewe, hatuwezi kusema kwa sababu amekosea basi aadhibiwe, tunaishi katika jamii ambayo watu wana matatizo. Aliendelea na kusema  "Niseme tu watu tusizungumze tu ili tuonekane kwenye runinga, nadhani ni vema tukafikiria kwa mapana na vizuri zaidi" Hapa alikuwa akimzungumzia Tundu Lissu ambaye sidhani kama pana mtu anaweza akasema kaenda bungeni kuuza sura kutokana na mchango wake mkubwa katika bunge hili, sasa hii ni kama Werema anaudhiwa na udadisi mkali na wa haki wa Bw Lissu ambaye kwa hakika amekuwa mwiba mchungu kwa serikali kwa ujumla bungeni humo. 

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :