News
Loading...

Dhihaka na kejeli Bungeni!


Mh Zitto Kabwe Mb
Kauli ya Bw Werema iliyodai watu wanaongea ili wauze sura ilimfanya Zitto Kabwe aombe  mwongozo wa Spika na kusema " Mheshimiwa spika humu ndani sisi ni viongozi na tupo kwenye legislation process. Sasa kuna kauli za kuudhi zinazotolewa na Mh mwanasheria mkuu wa serikali hazivumiliki" Aliendelea Mimi namheshimu sana Bw Werema, lakini siamini hii kauli hizo ni zake, labda awe ameumwa siku mbili tatu hizi. Kusema wabunge hatufikiri sawasawa anatutukana wabunge, namuomba awaheshimu wabunge na aondoe kauli yake ya kuwa wabunge wanaongea ili waonekane runingani. Akitolea mwongozo suala hilo Spika Makinda alisema" Nashukuru kadri muda unavyokwenda wabunge mnaelewa kuna kauli zinazoudhi na wengine kauli hizo mnazitolea magazetini. Ni kweli kauli ya Jaji Werema inaudhi na tunamuomba aiondoe" Baada ya kauli hiyo jaji Werema akasimama na kusema" Mimi sijaumwa ni mzima kabisa" Baadaye Zitto akasimama na kusema " Nakubali jajai Werema hajaumwa, na nafuta kauli yangu" Sasa mwanasheria mkuu simama ufute kauli yako aligiza spika Makinda" Naitoa kauli yangu, alisema Bw Werema.

Sasa hali hii inasababishwa na chuki na dharau inayojengeka kidogo kidogo na hatimae tutakuja shuhudia masumbwi bungeni!
Spika naye anachombeza kwa kijembe kwa kauli yake kuwa anashukuru kuwa sasa wabunge wameanza kuona kuna kauli zinazoudhi tena wengine wanazotolea katika vyombo vya habari, Mh kazi ipo!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Anonymous said...

huyu mh.makinda anawabeba waliomuweka hapo alipo ccm, na nahisi amechaguliwa ili awavunje nguvu na kuwakatisha tamaa wabunge wapinzani pasi na kufuata katiba ama kweli CCM makwisha.!!!