News
Loading...

Mtatiro anapomlipua Mbowe!


Julius Mtatiro
Naibu katibu mkuu wa CUF Bw Julius Mtatiro akichangia mjadala wa Kiongozi wa upinzani bungeni Bw Freeman Mbowe kulikataa gari la kifahari alilopewa na serikali alisema " Anachokifanya Mbowe ni propaganda za kisiasa zenye lengo la kumpatia umaarufu. aliongeza Mbowe ni kiongozi wa upinzani bungeni, amepewa gari na serikali kwa shuhuli hiyo, analirudisha gari kwa sababu yeye ni tajiri, angekuwa hana uwezo kama wabunge wengine angelirudisha? Alihoji Mtatiro. Mtatiro alisema Mbowe asijifanye anawahurumia wa Tanzania masikini, wakati maisha anayoishi ni ya kifahari yasiyofanana na wananchi wa kawaida.

Mtazamo wangu ni:
Kama Mbowe anajifanya au ni kweli anatuonea huruma wa Tanzania masikini alilofanya  la kuikataa gari hilo kwa kuwa yeye ni tajiri basi ni jambo jema, kwani hatua yake hiyo itaokoa pesa za umma na hatimaye pesa hizo kupelekwa katika taasisi nyingine kama afya, elimu na barabara, hivyo basi hatua hiyo ya Mbowe ni ya kuigwa na viongozi wengine na kama atapata umaarufu kupitia suala hilo basi umaarufu huo ataupata kwa haki kabisa. Hongera bwana Mbowe!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :