News
Loading...

Kamishna Chagonja naye aelewe wakati wa kampeni bado!


Kamishna Paul Chagonja


Kauli ya Kamishna Chagonja nilivyonukuu toka gazetini
Nimesoma magazeti ya The African na Habari leo ya tarehe 7.Juni.2011, humo kuna habari kuwa Kamishna wa Oparesheni na mafunzo waJeshi la Polisi Paul Chagonja akijibu swali kuhusu kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Bw Freeman Mbowe, alisema  katika HABARI LEO "kitendo alichokifanya Mbowe kinauonesha umma wa Watanzania udhaifu alionao na kueleza kuwa kiongozi wa aina  hiyo ni wa kugopwa, kwa sababu atakuwa analea wananchi katika misingi ya kuvunja sheria. Na kwenye The African alikaririwa akisema "The country under CHADEMA will be chaotic baecause leaders lack role model and their followers had been created so and they will devolope like wise.

Mtazamo wangu:
Kwa kauli alizozitoa dhidi ya CHADEMA na Freeman Mbowe ni ya kusikitisha hasa kutoka kwa askari mwenye cheo kama chake, labda na yeye hajui kuwa wakati wa kampeni bado kwani inaelekea dhahiri anakipigia kampeni chama fulani ambacho sina haja ya kukitaja nyote mnakijua. Pia ni dhahiri anajiingiza katika siasa ambapo yeye kama askari hapaswi kuonesha mwelekeo wake kisiasa lakini hii ndio Tanzania inayoadhimisha miaka 50 ya uhuru baadae mwaka huu, unategemea nini zaidi?

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :