News
Loading...

Kuzimika kwa umeme uwanja wa Taifa Jumapili, Tume ya nini?


Leo hii asubuhi nimesoma kuwa Waziri wa Utamaduni Bw Emmanuel Nchimbi ametangaza kuunda tume ya kuchunguza kwa nini umeme ulizimika uwanjani

Mh Emanuel Nchimbi

Sasa jamani hebu tuokoe pesa za mlipa kodi kwanza, nchi si inafahamika ipo katika tatizo la umeme? Labda cha kuangaliwa hapo ni kwa nini generator hazikuwaka umeme ulipokatika? na hili sioni kwamba linahitaji tume. Cha msingi ni kuwa mhusika kimkute kilichomkuta Bw Florian Kaijage aliyekuwa afisa habari wa TFF pale CD ya wimbo wa Taifa iliponasa huku Mh Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akiwepo uwanjani Taifa stars ilipocheza na Morocco mwaka jana. Mimi binafsi sina tatizo na TANESCO tunaelewa wanakabiliwa na changamoto gani, lakini serikali ya Tanzania nina tatizo nao kubwa tu, wakijua tupo katika tatizo la mgawo wa nishati ya umeme na hawakujiandaa na katikizo iwapo lingetokea kama ilivyotokea. 


Hivi karibuni mjini Tabora kuna vijana waliandaa tamasha la vyuo na shule za sekondari wakaliita SECOCOLLEGE BASH, wakaalika wasanii wazuri tu wa Bongo Flava wakiwemo Nguli 20percent, Juma Nature, Belle9 na Samir show ilifanyikia katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi watu wakajaa kwa bahati mbaya show ikielekea mwisho huku Juma Nature hajatumbuiza umeme ukakatika. Na kwa bahati mbaya tena vijana wale walisahau kuweka standby generator pale uwanjani hivyo show ikasimama huku kiza kikiingia. Kwa bahati vijana wale wakapata generator la kukodi na Juma Nature akatumbuiza na show ikaisha kwa usalama. Je? Serikali na ukubwa wake wote na mapesa waliyonayo inaonaje ikifananishwa na vijana hao wa Tabora? 

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :