News
Loading...

Marekani yazuia msaada wa dola milioni 800 kwa Pakistani


Rais Barack Obama ameamrisha kusitishwa kwa msaada wa dola milioni 800 kwa jeshi la Pakistani, mnadhimu mkuu wa serikali ya Obama alisema jumapili ya jana, wataalamu wamesema hatua hiyo ni katika kuibana Pakistani katika vita dhidi ya Ugaidi 
Afisa mwandamizi William Daley ameueleza uhusiano kati ya US na Pakistani kuwa wenye utata mwingi na ambao lazima ufanyiwe kazi ya ziada lakini akaongeza mpaka tutakapopita kipindi hiki kigumu na matata tutaendelea kuzuia pesa za walipa kodi wa kimarekani kwenda Pakistani.
Kusitishwa msaada kwa Pakistani kwanza kuliripotiwa na gazeti la New York times na kufutiwa na taarifa ya  Mnadhimu mwenza Bw Mike Mullen, kuwa kitengo cha ulinzi cha Pakistan kili idhinisha kuuawa kwa mwadishi wa habari aliyeandika juu ya kuwemo askari wenye siasa kali ndani ya jeshi la Pakistani.
Tuhuma ambayo ilikanushwa vikali na viongozi wakuu wa Jeshi la Pakistan, pamoja na idara ya Intelijensia ya nchi hiyo ambayo imekuwa na uhusiano wa kihistoria na kundi la Taliban na makundi mengine ya aina hiyo.
Bw Daley, amehojiwa karibuni na runinga ya ABC akasema kuwa uamuzi wa kusitisha msaada kwa Pkistan umechagizwa hasa na nchi hizo mbili kutokuwa na uhusiano mzuri tangu Marekani walipovamia Abottabad na kumuua kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida Osama Bin Laden.
Akaongeza"Kwa vyovyote bado wana maumivu kuwa tulimpata Bin Laden"
Tangu kuuawa kwa Bin Laden mahusiano kati ya nchi mbili hizi yamezorota mno kiasi cha kutia shaka na nafikiri tutaendelea kuona na kusikia mengi toka kwao.


Habari hii ni kwa msaada wa mtandao

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :