News
Loading...

Tusiwalaumu TANESCO!


Tatizo la giza linaloendelea kututesa wa Tanzania kwa karibu miaka 7 hivi, kwa mtazamo wangu tatizo hili lilipofikia si vema sana kuwalaumu TANESCO kwani wao wamebebeshwa tu mzigo na serikali kupitia wizara husika. Tangu serikali ya awamu ya kwanza walijua kuwa mahitaji ya umeme yanaongezeka kadri muda unavyosogea lakini hawakuchukua hatua zozote kulinusuru taifa hili karimu na endekezi na penda amani.na giza lililotanda sasa katika miji yetu. Tuna njia kadhaa mbadala wa kutegemea mvua kuvuna umeme ikiwemo gesi na hasa makaa ya mawe ambayo hivi karibuni imefahamika kuwa tuna hazina ya kutupatia umeme wa kutosha kwa miaka mia na sitini bila shaka yeyote. Labda ndio desturi ya wa Tanzania hatuna mipango yeyote kwa future, mfano ni Timu zetu hazifanyi vema katika mashindano makubwa lakini tumeendelea kuajiri makocha wa kigeni wenye kulipwa mamilioni ya shilingi bila kuona au pengine ni kufumbia macho kuwa tunapaswa tuwajenge watoto tangu wakiwa wadogo. Hivyo basi mzigo huu si wa TANESCO bali viongozi wetu ambao labda walisahau sisi ndio mabosi zao sio wao wanaokwenda kwa ving'ora.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

tz biashara said...

Mkala natumai unapata nafuu kwa sasa.Naomba kukuuliza kama mtu ana tangazo ni kiasi gani unamcharge.Mimi ninatatizo kubwa kidogo na nilikuwa na kaprojecti kangu ktk shamba langu lakini kutokana na matatizo inanibidi niuze kinu cha kuzalisha umeme kwa kutumia upepo.Hiki ni kinu cha kuzalisha umeme K.W.75 na katika nyumba unahitajika K.W.5 au K.W.10 tu sasa huo umeme wa K.W.75 ni mwingi ambao unaweza kuuza au ama ukatumika ktk kiwanda cha wastani hutegemea na mashine ukubwa wake.Na kinu hiki uzuri wake ni utatumia tangaboi yaani (wind turbine)umeme wa upepo na sio mafuta kama kawaida ya generatorna hivyo utagharamia mwanzo na baadae hutokuwa na gharama yeyote kwani utategemea upepo tu na kusahau TANESCO.Tafadhali ingia ktk blog yangu utakiona pamoja na maelezo.

Mkala26 said...

Nashukuru Mungu asante sana, sintokuchaji chochote ukitokea umepata mteja utanifikiria tu. Blog yako inaitwaje? mkala26@yahoo.com

tz biashara said...

Asante sana Mkala,inaitwa biashara na matangazo lakini kama uta click hiyo tz biashara basi utaipata humo.