News
Loading...

YANGA BINGWA KAGAME CASTLE CUP 2011


Kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa Kagame Castle cup 2011

Mwali akisubiri kubebwa.
Timu ya Yanga leo imefanikiwa kutwaa taji la ubingwa Afrika Masharki na kati Kagame Castle Cup katika uwanja wa Taifa jijini Dar jioni hii. Baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika dakika 90, ziliongezwa dakika 30 ambapo super sub Mghana Keneth Asamoah aliipatia Yanga bao la ushindi mnamo dakika ya 109. Yanga ilifanikiwa kulinda goli hilo moja mpaka mpira ukaisha pamoja na Simba kutishia mara kadhaa. Yanga oyeeee!
Aibu ya mwaka mara ulipofikia muda wa kukabidhi kombe kwa washindi umeme ukakatika uwanjani huku ikielekea hakukuwa na Back up generators hivyo waziri wa utamaduni bw Nchimbi akatoa zawadi kwa Yanga huku akimulikiwa na Ambulance iliyokuwa hapo uwanjani. Aibu hii imekwenda mbali safari hii kwa Super sports walionesha mchezo huo dunia nzima na star tv walionesha mchezo huo Afrika nzima, labda serikali sasa itajipanga na suala la umeme.

Kikosi cha Simba sports club.
Picha kwa hisani ya michuziblog

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :