Kiungo wa kimataifa wa England Owen Hargreves anatarajiwa leo hii kujiunga na Man city ambao ni mahasimu wa timu ya zamani ya Hargreves Man united ambayo alijiunga nayo mwaka 2008 lakini akashindwa kuichezea timu hiyo ya Old Trafford mara nyingi kama ilivyotarajiwa baada ya kuwa majeruhi mara kwa mara na kujikuta akiichezea timu hiyo mara 39 tu katika misimu minne aliyokuwa hapo, ilihali akipokea mshahara wake kamili. Hali hiyo ilipelekea Man united kumuachia huru katika msimu huu, ndipo Hargreves akaamua kutafuta timu nyingine ambapo inaelekea msimu huu ataitumika Manchester City baada ya kupasi vipimo vya afya.
Unalikumbuika bango hili? |
Kujiunga kwake na Man city huenda kukamfanya awe adui mkubwa wa mashabiki wa Man united na hasa pale Man city watakapoamua kuweka bango la kumkaribisha Manchester kama hilio hapo juu ambalo waliliweka baada ya kumsainisha Carlos Tevez
0 comments :
Post a Comment