News
Loading...

Fabio Capello aambiwa asiongelee suala la John Terry


Fabio Capello
Kocha mkuu wa timu ya soka ya England Fabio Capello ameonywa na Metropolitan Police kuwa aache kuongelea kesi anayoshutumiwa nayo nahodha wa Chelsea na England John Terry ambapo anashutumiwa kutumia maneno ya kibaguzidhidi ya Anton Ferdinand ambapo ushahidi wa picha mwendo za sky tv zimemuonesha Terry akisema F****** Black C*** katika mchezo wa Queens Park Rangers dhidi ya Chelsea mwezi uliopita. Capelo amekuwa akilizungumzia mno suala hilo kiasi kwamba Met Police wamefikia hatua ya kumshtaki Capello kwa chama cha soka ch England FA kuwa aache kutoa maoni yake katika kipindi hiki ambacho wao Met Police wanalichunguza suala hilo. Habari mpya zilizopo tangu jana ni kuwa Anton Ferdinand amepokea vitisho vya kuuawa kufuatia msimamo wake wa kulalamikia kauli ya John Terry na Met Police wanalipa umuhimu wa juu suala kitisho hicho na wanalichunguza pia.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :