News
Loading...

Hatimaye Eugene Matipa azikwa na umati mkubwa Tabora


Eugene (Matipa) Engelbeth Kiwele
Born 05-Sep-1973 Died 05-Nov-2011
Hatimaye rafiki mpendwa Eugene (Matipa) Engelbeth Kiwele alizikwa siku ya jumapili katika makaburi ya Luhanzali nje kidogo ya mji wa Tabora ambapo umati wa watu wapatao 3000 ulihudhuria mazishi yake. Matipa ambaye alifariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu aliwahi kufanya kazi katika Mamlaka ya Tumbaku mkoani humo na hasa wilayani Urambo kabla ya kuacha kazi katika mamlaka hiyo Mwishoni mwa mwaka jana. Moyo wake ulikuwa na tatizo la kuwa mkubwa (Heart Enlargment). Ipo siku niliwahi kumtafuta kwa simu hakupatikana na baada ya siku kadhaa tulikutana akanambia " Dah kaka huu moyo ipo siku utakuja kuniua, yaani jana na juzi nimeumwa hadi kuongea na simu nikawa siwezi nikaamua kuzizima tu" Hapa inaonekan alijua tatizo lake la moyo lilikuwa kubwa na ambalo lingeweza sababisha kifo chake kama ambavyo imetokea. Mungu ailaze roho yake pema peponi! AMEN!

Hapa ndipo ilipofikia kikomo safari ya Matipa
ambapo ametutangulia nasi tu nyuma yake.
Waombolezaji wakisubiri kwenda mazishini

Hapa ni Neshno nyumbani kwa
wazazi wa Marehemu Matipa
Kina mama waombolezaji nyumbani kwa marehemu Matipa


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :