News
Loading...

Wito kwa Blatter kujiuluzulu wazidi baada ya kudai hakuna ubaguzi wa rangi katika mpira wa miguu


Eti unasema kuna ubaguzi katika soka?
Rais wa FIFA Sepp Blatter amejikuta katika maji ya moto baada ya kudai kuwa hakuna ubaguzi katika mchezo wa mpira wa miguu duniani ilihali nchini England kuna kesi mbili zinachunguzwa huku mmoja wa watuhumiwa wa kesi hizo mshambuliaji wa Liverpool Fc akiwa amefunguliwa mashitaka na chama cha soka chini humo na Met Police baada ya uchunguzi wao kukamilika na kuona Luis Suarez ana kesi ya kujibu kufuatia tuhuma dhidi  yake kutoka kwa Patrice Evra ambaye alidai kuwa Louis Suarez alimwita Negro au negrito kwa mara zisizopnugua 10 katika mchezo kati ya Liverpool na Man united  katika dimba la Anfield mwezi wa Oktoba. Blatter aliulizwa na televishoni ya CCN anafikiri kuna ubaguzi katika soka? Naye alijibu " Nakanusha, hakuna ubvaguzi katika soka.  Labda mchezaji mmoja amemuita mchezaji mwingine neno ambalo si sahihi, lakini pia yule aliyeathirika anapaswa aseme tupo mchezoni, baada ya mchezo tutapena mkono na yatakuwa yamekwisha.Kutokana na kauli yake hiyo imetafsiriwa kuwa Blatter haoni kama kuna umuhimu wa kutokomeza kabisa ubaguzi wa rangi katika soka, hasa ukizingatia yeye ni rais wa FIFA. Nchini England ambako tayari kesi mbili zinaznguruma kwa sasa pamekuwa na wito kumtaka Sepp Blatter ajiuzulu wadhifa wake huo.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :