News
Loading...

Ian Wright agomea kutoa tuzo kwa mchezaji bora wa dunia!

Ian Wright nguli wa Arsena na England.

Ian Wright amesaema hatohudhuria sherehe za Ballon D'Or awards ambapo hutajwa mchezaji bora wa dunia zitakazofanyika mapema mwakani, Ian Wright aliombwa na Sepp Blatter akabidhi mpira huo wa dhahabu kwa mshindi mapema mwakani. sherehe hizo zitakazohudhuriwa na wacheza mpira maarufu akiwemo Pele, Ronaldo,Becham na Ronaldo kwa kutaja wachache. Kutohudhuria kwake kunasababishwa na kauli ya rais wa FIFA Sepp Blatter ambaye alidai mchezaji akibaguliwa uwanjani mwisho wa mchezo ampe mkono aliyemdhalilisha na yawe yamekwisha.

Ian Wright anasema"Nilipoombwa kukabidhi ballon d'or, niliona ni kama ndoto iliyokamilika nakuwa kitu cha kweli" akaongeza "Lakini nasikitika kuwa kama hatoomba msamaha ambapo na akiomba msamaha pia itabidi ajiuzuru wadhifa huo, mimi sitokwenda kukabidhi zawadi hiyo. 

Blatter: Mimi si mbaguzi umeona nimepiga picha na mtu mweusi

Fifa baada ya kuona Rais wao anaandamwa wakaposti picha yake na Tokyo Sexwale ambaye ni mtu mweusi aliyefungwa na utawala wa kibaguzi Afrika kusini kana kwamba kujikosha kuwa yeye si mbaguzi. Lakini Blatter ameshaumiza watu wengi kwa kauli yake hiyo na ni vema ajiuzuru tu!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

Anonymous said...

Kaka nadhani unapinga sana ubaguzi wa rangi, ni vizuri sana. Nakumbuka hata huko nyuma ulitoa idadi ya makocha wa Ligi Kuu ya England kama sikosei ulikuwa unaangalia idadi ya weusi na weupe. UBAGUZI NI MBAYA...

Lakini ngoja mimi niende mbali kidogo...alichosema Blatter ni kuwa ndani ya uwanja wachezaji wanaweza kusemeana maneno fulani fulani and not necessary racist comment...then wanapeana mikono inakuwa mwisho wake....Nimefurahi nilipoona ame apology na kuelezea alichokuwa anasema...

Racism hipo sehemu zote duniani ni wajibu wetu kuupinga ubaguzi huu..kuna Russian Psychologist aliyesema...kuwa kuna chembe ya ubaguzi karibu kwa kila mwanadamu...

Nakumbuka hata Tanzania miaka iliyopita kuna dada wa kihindi alishinda Miss Tanzania watu walipinga sana....hata kwetu Tabora utasikia watu...huyu Muarabu, huyu mchaga.....tunawabagua watu kwa makabila sababu ya kufanyikiwa kwao...

Mkala Fun said...

Nashukuru kwa maoni kaka. Unajua inawezekana Luis Suarez,John Terry na Sepp Blatter wotw si wabaguzi wa rangi ila kauli walizotumia ni za kibaguzi. Nakumbuka Mwl Nyerere aliwahi kusema "dhambi ya ubaguzi ni kubwa sana, ukianza kumbagua mtu kwa kuwa yeye ni CCM au CHADEMA kisha wale uliobaki nao utataka kujua kabila zao kisha utawabagua na wao kisha mkishabaki na kabila lako tu utataka kujua dini zao, kisha nao utawabagua. Nafikiri alichotaka kumaanisha ni kuwa ubaguzi hauna mwisho! Hivyo ni bora tupigie kelele huu wa rangi. Mimi niliathirika na ubaguzi wa rangi wakati nikiishi England. Hivyo naelewa wanavyojisikia wale wanaolalamika kubaguliwa kirangi! Ahsante!