News
Loading...

Sheria moja maamuzi mawili tofauti



Jengo la Madrasa lililosimamishwa.
Katibu mtendaji wa kata ya Mwananyamala Bi Florah Mizengo amezuia kuendelea kwa ujenzi wa Madrasa (pichani) katika eneo la wazi (Open space) lililopo katika viwanja vya Kinondoni Msufini, ujenzi huo uliokuwa ukifanywa kwa ufadhili wa baadhi ya wakazi wa eneo hilo inasemekana umefanywa kinyume na makubaliano ya kati ya walimu wa madrasa na mtendaji wa serikali ya mtaa wa Msisiri Bw Kijoh vilipo viwanja hivyo ambaye anaelezwa aliwaruhusu walimu wa madrasa hiyo wajenge msingi wa matofari lakini juu wamalizie kwa mbao kwa kuwa viwanja hivyo ni vya wazi na haparuhusiwi kujengwa majengo ya kudumu. Lakini katika hali isiyoeleweka walimu hao wakaamua kujenga kwa matofari mpaka kiasi kionekanacho pichani na kupelekea Mtendaji wa kata ya Mwananyamala kusimamisha ujenzi huo. Kwa upande wao walimu wa madrasa hiyo wamekuwa wakilalamika kwa nini wao wazuiwe kujenga jengo la kudumu ilihali pahala hapo palikuwa na jengo jingine la kudumu lililomilikiwa na umoja wa kinamama wa CCM? Na ukitazama hilo ni kweli walimu hao ubishi wao una mashiko, kwani kuna mfano mzuri na hai katika mtaa huo huo wa Msisiri A ambapo CCM imejenga maduka katika uwanja wa wazi lakini hakuna hatua yeyote inayochukuliwa dhidi ya chama hicho tawala si na serikali ya mtaa wala ile kuu kupitia wizara ya ardhi. Kwa mtazamo wangu tu ni kuwa hakuna taasisi yeyote inayopaswa kuwa juu ya sheria za nchi, iwe serikali, CCM au madrasa wote hawa hawapaswi kujenga katika maeneo ya wazi, umefika wakati waziri wa ardhi aache unazi na avunje majengo yote ya CCM yaliyopo katika maeneo ya wazi!



Kushoto ni nyumba zinazozibwa na majengo ya CCM Msisiri
Hii ni ofisi ya CCM Msisiri iliyojengwa katika eneo la wazi


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :