News
Loading...

Uhuru wa vyombo vya habari hatarini Tanzania


Absalom Kibanda akiwa ICU MOI.
Ni dhahiri kuwa hakuna uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania, tena basi katika nchi inayoitwa KISIWA CHA AMANI, na hilo linathibitishwa na unyama wanaofanyiwa wahariri na waandishi wa habari hapa nchini.

Mahututi
Kufuatia kutekwa na kupigwa kinyama Bw Absalom Kibanda ambaye ni mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF ni dhahiri kuwa Tanzania imekuwa nchi inayoelekea katika vitendo vya kimafia, maarufu nchini Italy. Katika miaka isiyozidi mitatu tumeshuhudia kumwagiwa tindikali Said Kubenea wa Mwahahalisi kulikofanywa na watu wasiojulikana, kuuawa kwa Mwandishi David Mwangosi mkoani Iringa kwa kufyatuliwa bomu la machozi tumboni na askari wa kikosi cha FFU, mtumishi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Na kupigwa vibaya, kung'olewa kucha na meno kwa Dkt Ulimboka ambaye alikuwa kiongozi wa umoja wa madaktari waliogoma mwaka jana. Dk Ulimboka alidai kumfahamu mmoja wa watu waliomshambulia kuwa ni afisa wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mungu Ibariki Tanzania!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :