News
Loading...

Posho za wabunge Utata!


Mh Mkulo-WaZiri wa Fedha
Wabunge wa CHADEMA wanaelekea kupata ushindi wa vita ya ki saikolojia dhidi ya wenzao wa CCM mara baada ya wabunge wa CHADEMA kuamua kusamehe posho zao za vikao na kuitaka serikali kupitia hazina izifute posho hizo zinazofikia sh 150,000 kwa siku na kikao kimoja na zielekezwa kwingine penye mapungufu. Wabunge hupata mshahara wa sh 2,500.000 kwa mwezi pesa hizo zikichanganywa na posho ya mafuta na ghrama za uendeshaji wa ofisi hufikia 7.2m kwa mwezi. Kikao hiki cha bunge kinachoendelea kitagharimu serikali sh 2.52 Bilioni.

Zitto Kabwe: Pesa za posho ziende kwingine.

CHADEMA inadai pesa hizo zipelekwe katika sekta za Afya, Elimu na Barabara kitu ambacho ni kizuri  sana na kinaonesha kujali wananchi, lakini sijui mtazamo wa wabunge wa CCM upo vipi juu ya hilo? Vita hii naifananisha na zile hufanywa na Sir Alex Ferguson kabla ya mechi muhimu dhidi ya wapinzani wake maarufu kama MIND GAMES sasa wabunge wa CCM wakilipinga hilo si wataonekana hawawajali wananchi wao? Mind games!!!!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

Rik Kilasi said...

Hapo patamu ngoja tusikie CCM watasema nini.

Anonymous said...

Hili suala mi naliunga mkono, kwani sioni mantiki ya mbunge kulipwa perdiem ambayo ni haki yake kwa vile nje ya kituo cha kazi halafut tena alipwe posho ya kikao ambayo ndiyo kazi yake ya msingi. Kima cha chini cha mshahara Tsh. 120,000 halafu posho ya mbunge akiwa bungeni mbali na perdiem yake ni takriban 150,000. Kwa kweli serikali ya CCM ituonee huruma wanyonge, tunateseka ndani ya nchi yetu. Angalau tunakuwa na imani na hawa CHADEMA kwani wameonyesha mfano wa kutujali wananchi.

Anonymous said...

Dah hata la kusema sina, mimi ni hoi lakini ndio Tanzania yetu hii! Hopefully mind games za CHADEMA na Zitto zitatuvusha hapo.