News
Loading...

Yanga inapogoma kuvaa jezi zenye alama mpya ya Mdhamini wa ligi yaTanzania!


Kuna habari ambayo niliisoma miezi kadhaa iliyopita, habari hiyo ilinichekesha na pia kunishangaza pale kiongozi mmoja wa kilabu cha Yanga alipokaririwa akisema kuwa timu yake haitovaa jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu wa Ligi nchini yaani Vodacom Tanzania Limited ambao wamebadili nembo yao toka rangi ya bluu, kijani na nyeupe  na kuwa kama hivi.


Kilichonichekesha na kunishangaza ni kuona kuwa viongozi wa Yanga wanapoonesha kutokomaa ki biashara, kwa kuwa inaelekea itatokea klabu itamkataa mdhamini kwa kuwa nembo ya kampuni yake ni nyekundu. Sasa huku tunapoelekea mimi hata sipajui lakini kuna kila dalili kuwa si pazuri hasa katika ulimwengu wa soka la kisasa ambalo linaendeshwa ki biashara zaidi kuliko kufuata miiko ya Usimba na Uyanga. Natumai suala hilo halitoleta utata kati ya Yanga na TFF na Mdhamini kwani Yanga inaongozwa na Lloyd Nchunga ambaye ki taaluma ni mwanasheria. Vodacom Premier League 2011/12 imepangwa kuanza jumamosi ijayo tarehe 20/08/2011

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Anonymous said...

Brother wewe mwenyewe unasema tuache Usimba na Uyanga na wewe mwenyewe bado umebaki huko huko. Argument uliyoandika yaani ni weak kabisa. Yanga wana Kosa gani? Mkataba wa Vodacom si wa vilabu bali TFF na Vodacm.

Ligi kuu ya Uingereza inadhaminiwa na Barclays, Je timu za Uingereza zinavaa jezi zenye nembo ya barclays?

Mimi naona Yanga wapo sahihi, wanatakiwa kuwa na wadhamini wengine, udhamini wa vodacom ni kati yao na TFF.

Mkala26 said...

Ni kweli kuwa nilisema tuache uyanga simba ili soka letu lipige hatua. Na ukweli ni kuwa timu za England zinavaa nembo ya mdhamini wa English Premier ambao ni Barclays na nembo hiyo hukaa begani. Kwa hiyo Yanga wanakosea kuikataa nembo hiyo ya Vodacom.