News
Loading...

Kocha wa zamani wa Ufaransa aiita Manchester United klabu ndogo!



Kocha wa zamani wa Ufaransa Raymond Domenech amemuasa golikipa wa Totenham Hotspurs Hugo Lloris asijiunge na Man United kwa kilabu hicho cha jijini Manchester kwa sasa hakina hadhi kuitwa kikubwa, kauli ambayo imepingwa na wengi nikwemo mimi. Domenech ambaye alimpa Lloris mchezo wa kwanza Lloris mwaka 2008 Ufaransa lilipocheza na Uruguay alisema "Lloris anapaswa ahame Totenham na akacheze katika kilabu kikubwa kinachocheza michuano ya ubingwa wa ulaya na kilabu hicho kiwe Chelsea, Man city au Arsenal lakini si Man united" akaongeza "Kwangu mimi Man united si timu kubwa tena, ipo sawa na Totenham hivyo ndivyo ninavyofikiri"  Hivyo anapaswa aende akacheze katika vilabu vikubwa vya England, Spain, Italy au hata Ufaransa.

Mashabiki wa soka nikiwemo si tu tunakataa kwamba Man united ni klabu ndogo bali pia tunajiuliza alikuwa katumia ulevi gani siku ya mahojiano hayo?

Ukweli ni kuwa Man united anayoiita timu ndogo katika misimu miwili iliyokosa ubingwa 2013/14 na 2014/15 ilikuwa misimu ya mpito 2013/14 Baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu akamuachia timu David Moyes aliyefanya vibaya mpaka timu ikamaliza msimu ikishika nafasi ya 7 na 2014/15 Louis Van Gaal akapewa timu hiyo akija na fomesheni mpya na mbinu tofauti za ufundishaji, hivyo ikawa vigumu kufanya vema katika ligi hiyo ngumu ya EPL.

Ukiangalia timu anazoziita kubwa zote ukiindoa Chelsea hazijawahi hata kushinda kombe hilo la Ulaya na katika, Arsenal ikicheza fainali 2006 na kuendelea kuboronga katika michuano hiyo huku Man city wakiwa kichwa cha mwendawazimu katika michuano hiyo na timu aiitayo ndogo ikicheza fainali 3 za michuano hiyo na kushinda mara 1. Na bado sifikirii unaweza iita Liverpool ni klabu ndogo kwa kuwa haiajafanya vizuri karibuni.     
Hugo Lloris wa Totemham Hotspurs
Timu ndogo Man United ilipocheza Real Madrid katika mechi za majaribio msimu uliopita jijini Ann Bhor ktk uwanja wa Michigan mwaka 2014 mchezo huo uliingiza mashabiki laki 109 na kuvunja rekodi kwa mchezo wa soka Amerika.

Habari na picha kwa hisani ya mailonline Imefasiriwa na Mkala Fundikira

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :